Njia ya kuhifadhi Qur-aan


Swali: Nielekeze katika njia ambayo itanisaidia kuhifadhi Kitabu cha Allaah?

Jibu: Tunakuusia kutilia umuhimu kuhifadhi na kuliekea jambo hilo. Chagua muda munasibu wa kuhifadhi kama mwishoni mwa usiku, baada ya swalah ya Fajr au katikati ya usiku au katika nyakati nyenginezo ambazo nafsi inakuwa imepumzika ili uweze kuhifadhi. Pia tunakuusia kuchagua rafiki mzuri ambaye atakusaidia kuhifadhi na kujikumbusha. Sambamba na hayo mwombe Allaah mafanikio, msaada na kumlilia akusaidie, akuwafikishe na akulinde kutokamana na sababu za mikingamo. Yule ambaye anamtaka msaada Allaah kikweli basi humsaidia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/293)
  • Imechapishwa: 20/02/2021