Kuswali ´Ishaa nyuma ya anayeswali Tarawiyh II

Inajuzu kwa mtu kuswali swalah ya faradhi nyuma ya ambaye anaswali swalah ya Sunnah. Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema kwamba mtu ambaye amepitwa na swalah ya ´Ishaa na akaiswali nyuma ya anayeswali Tarawiyh, hakuna neno. Kujengea juu ya haya tunasema kitendo hichi ambacho hufanywa na baadhi ya watu – kama alivyosimulia muulizaji – kinafaa. Mtu akija na akakuta ameshapitwa na swalah ya ´Ishaa na akawakuta wanaswali Tarawiyh, inafaa kwake kujiunga pamoja nao kwa nia ya kuswali ´Ishaa. Kila mmoja atalipwa kwa kile alichonuia. Pale imamu atapotoa salamu kumaliza Tarawiyh, basi atakamilisha yale yaliyobaki katika swalah yake ya ´Ishaa. Kama amewahi Rak´ah mbili atakamilisha Rak´ah mbili. Kama amewahi Rak´ah moja atakamilisha Rak´ah tatu.

Kitu ambacho najizuia kusema neno ni kule kumsubiri kwao imamu na pale anapoanza kuswali Rak´ah mbili zengine wanaendelea naye na kukamilisha swalah pamoja naye. Jambo hili mimi nanyamaza. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kile mtachowahi swalini na kile kitachokupiteni kikamilisheni.”

Udhahiri wake ni kwamba mswaliji anatakiwa kukamilisha kivyake kile kilichompita pamoja na imamu wake. Akamilishe peke yake. Kwa msemo mwingine asisubiri mpaka pale imamu atapotoa salamu ya pili. Hapana, asifanye hivo. Tunasema imamu akitoa salamu ndani ya swalah ile aliyomuwahi, basi wewe kamilisha. Usisubiri mpaka pale atapoanza tena kuswali swalah nyingine.

Swali: Kwani swalah yake imemalizika kwa kutoa salamu. Ni vipi huyu imamu atakata swalah yake na huyu bado amebaki akimsubiria imamu?

Jibu: Hiki ndio ninachomaanish. Ndio maana nikasema kuwa mimi najizuia. Haitakikani kwake kufanya hivo. Anachotakiwa kufanya pale imamu atapotoa salamu ambayo wamejiunga pamoja naye wakamilishe swalah zao kila mtu kivyake. Kisha ndio waswali pamoja na watu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (15) http://binothaimeen.net/content/6801
  • Imechapishwa: 21/02/2021