Swali: Ni kufuru kubwa kuwatukana Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum)?

Jibu: Akiwatukana kwa ajili ya juhudi zao na kwa ajili ya kumnusuru kwao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na dini, ni kufuru kubwa.

Ama akiwatukana kwa ajili ya kuchukia kitu kutoka kwao au akawa anamfuata kichwa mchunga mtu, ni dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa na sio kufuru. Hili ni kwa mtazamo wa mmoja mmoja.

Hata hivyo endapo atawatukana Maswahabah wote bila ya shaka ni kitendo cha ukafiri. Kuwatukana jumla ya Maswahabah ikiwa ni pamoja vilevile na Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na ´Aliy, wale Maswahabah kumi waliobashiriwa Pepo na Maswahabah wa vita vya Badr, waliotoa kiapo cha usikivu na utiifu chini ya mti na wale waliosilimu kabla ya Ushindi na wakahajiri, ni kufuru.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdah–14340316.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020