Swali: Ni vipi mtu anatubia juu ya kusengenya? Je, ni lazima mtu kumuomba msamaha yule aliyemsengenya?

Jibu: Kutubu ni yeye kuacha kusengenya. Ikiwa anajua kuwa yule msengenywaji atamkubalia msamaha wake amuombe msamaha. Na ikiwa anajua atakasirika na hatomsamehe, inatosheleza kwake kumuombea du´aa na kumsifu. Hili linatosha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdah–14340316.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020