Swali: Ni ipi hukumu mtu akivaa soksi hali ya kuwa na twahara baada ya Fajr na wakati alipokuwa anatawadha kwa ajili ya Dhuhr akapangusa juu yake. Baada ya kumaliza kuswali akavaa soski zengine juu yake hali ya kuwa niko na twahara. Je, inafaa kwangu kupangusa juu ya soksi zilizoko juu? Je, hukumu ya kumalizika kwa muda wa kupangusa inahusu soksi zilizoko juu au chini?

Jibu: Hapana vibaya kupangusa juu zile zilizoko juu ikiwa ulizivaa katika hali ya twahara na katika hali hiyo muda wa kupangusa utafungamana na zile zilizoko juu kwa sababu zilivaliwa katika hali ya twahara. Ni kama ambavo akivaa soksi za ngozi au za kawaida hali ya kuwa na twahara basi inafaa kwake kupangusa juu ya kitata[1].

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/21-ni-ipi-hukumu-ya-kupangusa-juu-ya-kitata/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/118)
  • Imechapishwa: 27/08/2021