Swali: Ni ipi hukumu ya Ruqyah na hirizi?

Jibu: Ruqyhah imewekwa katika Shari´ah ikiwa ni kwa Qur-aan, Majina ya Allaah mazuri na du´aa zilizowekwa katika Shari´ah pamoja na kuitakidi kuwa ni sababu tu na kwamba mwenye kumiliki madhara na manufaa ni Allaah (Subhaanah). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakuna neno kwa Ruqyah maadamu sio shirki.”

Ameipokea Muslim na wengine.

Vilevile (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwahi kusomea na yeye mwenyewe kusomewa.

Kuhusu Ruqyah iliyokataza ni ile inayoenda kinyume na tuliyoyasema. Hivyo ndivyo wamevyosema wanachuoni.

Kuhusu kuvaa hirizi haijuzu, sawa ikiwa ni hirizi ya Qur-aan au kitu kingine kutokana na jumla ya Hadiyth zilizothibiti juu ya hilo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (01/207)
  • Imechapishwa: 24/08/2020