Inajuzu kuswali nyuma ya imamu anayewaandikia watu hirizi?

Swali: Kuna mtu, ambaye ni imamu wa msikitini, anaandika hirizi. Je, inajuzu kuswali nyuma yake?

Jibu: Inajuzu kuswali nyuma ya ambaye anaandika hirizi ya Qur-aan na du´aa zilizowekwa katika Shari´ah. Lakini pamoja na hivyo haifai kwake kuziandika kwa kuwa haijuzu kuzivaa.

Ama ikiwa hirizi hizi zina mambo ya shirki hakuswaliwi nyuma ya yule mwenye kuziandika na ni wajibu kumbainishia ya kwamba ni shirki. Ambaye ni wajibu kumbainishia ni yule anayemfunza.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/212)
  • Imechapishwa: 24/08/2020