Ni ipi hukumu nikiswali katika safu ambayo imekatika?

Swali: Inajuzu kuswali katika safu ambayo haikuungana? Ni ipi hukumu nikiswali katika safu ambayo imekatika?

Jibu: Inajuzu kuswali katika safu iliokatika. Lakini lililo bora ni kuunganisha safu. Ukiswali katika safu na hukukamilisha safu ya kabla yake ni sahihi lakini hata hivyo umeenda kinyume na Sunnah. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kukamilisha kwanza zile safu za mwanzo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 25/10/2018