Je, tufaha na machungwa vinatakiwa kutolewa zakaah?

Swali: Je, tufaha na machungwa vinatakiwa kutolewa zakaah?

Jibu: Havitakiwi kutolewa zakaah. Zakaah inakuwa katika nafaka na matunda yanayoliwa na yanahifadhiwa. Ama kuhusu tufaha na machungwa havihifadhiki. Kadhalika inahusiana na mboga, tomato, karoti na vitu mfano wake katika mboga za kila siku ni vitu visivyotakiwa kutolewa zakaah. Zakaah inakuwa katika nafaka, matunda, tende na zabibu ambavyo vinaliwa na vinahifadhika pia.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 25/10/2018