Ndio maana Mtume akatumwa kwa watu wote


Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kila Nabii alikuwa akitumilizwa kwa watu wake na mimi nimetumilizwa kwa watu wote.”[1]

Kwa sababu Shari´ah yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kamilifu, iliyoenea na pana. Ndani yake mna manufaa na ni yenye kusilihi pasi na kujali wakati na mahali. Hakuna furaha na kufaulu pasi nayo. Yule ambaye atatafakari msingi yake mitukufu basi ataona kuwa ina mafanikio ya duniani na Aakhrah.

[1] al-Bukhaariy (335) na (438) na Muslim (521).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bahjat-ul-Abraar, uk. 84
  • Imechapishwa: 24/02/2021