Namna hii ndivyo jinsi Umm-ud-Dardaa´ alivyokuwa Faqiyhah


Kuna Umm-ul-Dardaa´ wawili; mkubwa na mdogo. Mdogo alikuwa ni mwanachuoni. Hata yule mkubwa pia alikuwa na elimu. Yule mdogo alikuwa ni mwanachuoni na Faqiyhah [mwanachuoni]. Allaah amrahamu na awe radhi naye. Ni vipi alikuwa Faqiyhah? Tunataka kujua sababu. Alilkuwa ni Faqiyhah. Alikuwa ameolewa na mume mwanachuoni na Faqiyh anayefanyia kazi elimu yake. Kama jinsi tulivyosema alikuwa ni Faqiyhah. Ni vipi alikuwa Faqiyhah sasa? Je, alikuwa akitoka na kutafuta elimu huko na kule? Haki za mume ziko wapi sasa? Ni lazima mume alikuwa akimfundisha ahli yake. Hili tumeliona kwa wanaume wengi. Wakati wanapowazungumzisha wake zao hawawazungumzishi kwa elimu. Unaweza kuona jinsi watu wanavyofaidika kutoka kwake elimu na ana elimu nyingi, wema na maelekezo, lakini anapokuwa na mke wake anatangamana naye kwa muafaka wa mambo ya nyumbani – chakula, kinywaji, haja na mfano wa hayo. Hili si sawa. Mtu wa kwanza unayetakiwa kumfunza na kumkinga na Moto ni mke wako. La sivyo usimlaumu yeyote isipokuwa nafsi yako mwenyewe.

Mke wa Abud-Dardaa´ alikuwa ni Faqiyhah. Ina maana yeye ndiye ambaye alikuwa akimfundisha. Unapozungumza na wake basi zungumza nao kwa elimu. Wape elimu. Waeleze hali za Maswahabah. Waeleze yale uliyosikia kutoka kwa wanachuoni. Kwa njia hiyo unakuwa ni mwenye kufikisha elimu. Inawezekana wanawake na familia pale mwanzoni wakapata uzito juu ya hilo. Lakini wakati mioyo yao inapoanza kujisikia vizuri basi itaanza kulainika. Kama jinsi unavyowaathiri wengine mara kumi basi kadhalika iathiri familia yako. Hata hivyo si sawa mwanaume akawa ni mwenye kuomba tu chakula, kinywaji na haja. Kwa kuwa mwanaume ataulizwa kwa kile alichokichunga:

“Kila mmoja wenu ni mchungaji na kila mmoja ataulizwa kwa kile alichokichunga.”

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aal ash-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.af.org.sa/en/node/3234
  • Imechapishwa: 19/09/2020