Ewe dada wa Kiislamu, tahadhari usiolewe na mzushi au Hizbiy!

Swali: Ipi hukumu ya mwanamke kuolewa na mwanaume Hizbiy kashikamana na mapote ya leo ya kipotofu?

Jibu: Nakwambia ewe binti yangu wa Palestina uliomtaja ni mtu wa Bid´ah mpotofu. Na hajaridhiwa dini yake. Kasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atapokujieni yule mnaemridhia dini na tabia yake muozesheni, msipofanya hivyo itakuwa mnaeneza fitina kubwa katika ardhi na ufisadi.” (Hadiyth ni Hasan)

Makusudio awe ni mwanaume mwema. Msiwaozeshe mabanati zenu watu hawa Hizbiyyuun wapotofu watu wa Bid´ah. Watawatoa katika Sunnah.

Ama ikiwa mwanamke aliolewa na mwanaume huyu kwa kutokumjua au alilazimishwa na familia yake kwa sababu miongoni mwa sababu, yatakikana kwa mwanamke huyo kuwa na subira na aangalie maslahi ya watoto wake na awe nae kwa hekima na awe na tahadhari nae.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.youtube.com/watch?v=tqfIoLvSqOU
  • Imechapishwa: 19/09/2020