Mwenye kufa katika shirki ndogo atapata uombezi?

Swali: Kukataliwa uombezi kwa washirikina kama ilivyopokelewa katika Hadiyth kunaingia pia yule ambaye alifanya shirki ndogo kwa mfano mwenye kuapa kwa asiyekuwa Allaah?

Jibu: Huyu ni muumini hatoki katika Uislamu. Ambaye yuko na shirki ndogo hatoki katika Uislamu. Kinachomaanishwa ni mshirikina mwenye kutoka katika Uislamu ndiye ambaye uombezi hautomfaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (07) http://alfawzan.af.org.sa/node/2122
  • Imechapishwa: 02/07/2020