Swali: Watoto wa washirikina watawaombea uombezi wazazi wao na watafufuliwa nao?

Jibu: Hapana, watoto wa washirikina ni wenye kuwafuata wazazi wao. Duniani watataamiliwa mu´amala kama wa wazazi wao. Ama kuhusu Aakhirah wanachuoni wametofautiana juu yao. Kauli yenye nguvu – na Allaah ndiye anajua zaidi – ni kwamba jambo lao liachiwe Allaah (´Azza wa Jall). Imesemwa kuwa watatumiwa Mtume na awape mtihani; mwenye kumtii Mtume huyo ataingia Peponi na mwenye kumuasi ataingia Motoni. Allaah ndiye anajua zaidi kuhusu mafikio yao.

Hata hivyo hawatowaombea uombezi wazazi wao. Mshirikina uombezi hautomfaa si kutoka kwa mtoto wake wala mtu mwingine. Uombezi hautomfaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (07) http://alfawzan.af.org.sa/node/2122
  • Imechapishwa: 02/07/2020