Swali: Kuna mwanamke anfanya kazi kama muuguzi kwenye hospitali. Inatokea wakati mwingine wakati wa swalah unatoka kwa sababu ya kazi. Je, inafaa kwake kukusanya kati ya swalah mbili?

Jibu: Hapana. Aswali hapo kazini. Ikiwa wako kundi la wanawake watengeneza sehemu ya kuswalia ambapo watakuwa wanaswalia. Wanatakiwa kuswali swalah kwa nyakati zake na wasifanye mchezo na swalah na kuzichelewesha kuziswalia nyumbani na mfano wa hayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (58) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16539
  • Imechapishwa: 23/09/2017