“Msiwashughulishe wasiokuwa wasomi mambo ya Tawhiyd na ´Aqiydah”


Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa haitakikani kuwashughulisha wasiokuwa wasomi na mambo ya ´Aqiydah kama mfano wa kuwaambia kwamba Allaah yuko juu ya mbingu na mengineyo?

Jibu: ´Aqiydah ndio jambo muhimu zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliikaa Makkah akiithibitisha ´Aqiydah kwa miaka kumi na tatu. Miaka yote hiyo aliitumia katika ´Aqiydah. ´Aqiydah ndio msingi wa dini.

Swali: Mwenye kusema hivi anazingatiwa ni katika wanachuoni?

Jibu: Hapana, hazingatiwi ni katika wanachuoni. Bali anazingatiwa ni katika wajinga.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 34
  • Imechapishwa: 09/11/2016