Swali: Kuna mtu ameoa mwanamke wa Kiislamu ambaye ana upungufu katika dini yake. Anasafiri bila ya Mahram. Mume alikuwa anajua hilo kabla ya ndoa. Je, amvumilie, kumfundisha na kumnasihi au atengane nae moja kwa moja?

Jibu: Mkataze. Una haki ya kumkataza kusafiri pasi na kuwa na Mahram au asafiri pamoja na wewe. Ni haki yako kumkataza kusafiri. Hana haki ya kusafiri bila ya idhini yako. Akiendelea kung´ang´ania mtaliki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (41) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%204%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 13/03/2017