Swalah ya mkusanyiko ni Sunnah kwa dalili hii?

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah ya mkusanyiko ni bora kwa daraja ishirini na saba kuliko anayeswali peke yake.”

Kuna wanaoitumia kama hoja kwamba swalah ya mkusanyiko imependekezwa tu. Je, utumiaji wao wa dalili ni sahihi?

Jibu: Hapana, si sahihi. Hadiyth inalenga tu fadhila za swalah ya mkusanyiko. Kuhusu hukumu yake inachukuliwa kutoka katika dalili zingine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kusikia adhaana na asiiendee hana swalah isipokuwa kama ana udhuru.” Kukasemwa: “Ni udhuru upi?” Akasema: “Woga au maradhi.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (41) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%204%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 13/03/2017