Mke amtii mume anayemwamrisha kuvaa suruwali?


Swali: Je, mume anaweza kumuamrisha mke wake kuvaa suruwali [nyumbani] kwake tu?

Jibu: Hapana, asimuamrishe hilo. Asimuamrishe hilo, kwa kuwa suruwali si katika mavazi ya wanawake khaswa katika jamii yetu hii. [Mume] akimpa ruhusa, atampa ruhusa katika hali nyinginezo zisizokuwa hizi na ataichukulia sahali katika kuivaa. Asimwamrishe mke wake kufanya munkari, amuamrishe kufanya mazuri.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.youtube.com/watch?v=kv7AedjU2P8
  • Imechapishwa: 07/09/2020