Swali: Je, Salafiyyah imekomeka kwa wanachuoni au ina wanachuoni?

Jibu: Lay Salafiyyah ingelikuwa imekomekana kwa vijana, basi ingelikuwa ni vuguru. Nenda Haram. Ni wangapi utaona wamekaa na Shaykh Ibn ‘Uthaymiyn? Utaona umati wa watu. Ni wangapi utaona wamekaa na Shaykh Ibn Baaz? Vijana wasiokaa na wanachuoni wamechanganyikiwa. Wanatumbukia katika kuruka mipaka na upotevu. Vijana ambao wamelelewa na wanachuoni wako kati na kati. Wanasimama kidete dhidi ya watu wa Bid´ah na kubainisha batili na upotevu wao. Hali kadhalika Shaykh al-Albaaniy na Shaykh Rabiy´.

Au unamaanisha wanachuoni kama ‘Abdullaah al-Ahdal ambaye haoni tofauti kati ya Hadiyth ambayo ni Muttaswil na ambayo ni Musnad, ambayo ni Mudhtarib na ambayo ni Marfuu’, ambayo ni Mursal na ambayo ni Mu’allaq? Unataka nimuainishe katika mwa wanachuoni? Kamwe maishani. Haijuzu kukaa pamoja naye. Ni muongo mbaya. Anatusemea uongo. Kwani ametuona tunapokea pesa? Kwani ametuona tunawasiliana na maadui wa Uislamu na wanasekula na kuwa sisi ni wapelelezi wao? Ni muongo anayejiunguza mwenyewe – na himdi zote ni Zake Allaah!

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 155
  • Imechapishwa: 22/04/2015