Jambo la kwanza kabisa, ni mfumo mpya ambao umetoka Delhi na sio Makkah wala al-Madiynah. Chimbuko lao ni kutoka India nchi ambayo imejaa ukhurafi na Bid´ah. Hata hivyo, katika nchi hiyo kuna Ahl-us-Sunnah ambao wameshikamana na Sunnah na mfumo sahihi. Mfano Ahl-ul-Hadiyth ambao ni wabora kabisa katika mikoa hiyo.

Asli ya kundi hili limetoka katika nchi hiyo iliyotajwa na mji huo uliotajwa. Limejengeka juu ya mambo maalum yaliyozushwa na mtu huyo huyo aliyezusha mfumo huu.

Muasisi wa kundi ni katika Ahl-ul-Bid´ah na mwanaharakati wa Suufiyyah ambaye yuko na ´Aqiydah mbovu. Ni Bid´ah mpya iliyozushwa. Katika wao kuna Suufiyyah na Ashaa´irah wasiofuata Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika ´Aqiydah na Manhaj.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamaad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jamaa´at-ut-Tabliygh fiyl-Qaarah al-Hindiyyah, uk. 448-449
  • Imechapishwa: 22/04/2015