Mbona bado twaona maasi yakifanywa licha kwamba mashaytwaan wamefungwa minyororo?

Swali: Ikiwa majini yanafungwa Ramadhaan, kwanini tunaona maasi katika mwezi wa Ramadhaan, au majini hufungwa mpaka anapofuturu aliefunga kisha yanafunguliwa? Mtume (swalla Allaahu ´alyhi wa sallam) anasema kama ilivyo katika Swahiyh:

“Inapoingia Ramadhaan, hufunguliwa milango ya Pepo na hufungwa milango ya Moto na Mashaytwaan hufungwa.”

Jibu: Imekuja katika swahiyh Ibn Khuzaymah kuwa ni yale Mashaytwaan wakuu ndio wanafungwa. Ama vile vidogo haviachi kuwasumbua watu na kuwafanyia uadui na maudhi. Kilichobaki pia ni nafsi yako. Baadhi ya nafsi huenda zikawa ngumu na inakuwa ndio sababu ya kutumbukia katika fitina na si shaytwaan, khaswakhaswa  walao mirungi. Inapofika wakati wa ´Aswr ngumi na matusi ni wao, muhimu ni kujiepusha na walao mirungi baada ya ´aswr…

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbil.net/fatwa.php?fatwa_id=1173
  • Imechapishwa: 19/05/2020