Maulidi ya Mtume na ya waja wema yanayofanywa Tanzania

Swali: E: Sisi Tanzania tunatengeneza chakula na tunakusanyika sehemu maalum ndani ya nchi na tunasema kuwa matembezi haya yanatokamana na mtu fulani kutoka katika pote la Qaadiriyyah ambaye ni ´Abdul-Qaadir. Je, kitendo hichi ni katika Bid´ah au ni katika Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Je, kina madhambi? Kwa sababu hatuimarishi misikiti mpaka kwanza kufanywe matembezi haya na kusoma Maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kufanya sherehe kubwa kwa sababu hiyo. Je, mambo haya yana madhambi au hapana?

Jibu: Katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah zake na Salaf-us-Swaalih hakupatapo kufanywa walima wala chakula juu ya maiti mwema aliyefariki. Hakuna Swahabah yeyote wala Salaf-us-Swaalih aliyesherehekea Maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika uhai wake wala baada ya kufa kwake. Vilevile hawakufanya chakula baada ya kufa kwake.

Kwa hivyo kufanya Maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), mtu mwema miongoni mwa watu wema au viongozi, mtu akasherekea hilo, kukasomwa yaliyoandikwa wakati wa kuzaliwa kwake, waliohudhuria wakasimama wakati kunapotajwa mazao yake kwa madai ya wenye kuhudhuria ya kwamba [mtu huyo] amekuja katika wakati huo, kufanya chakula kwa ajili ya kusherehekea Maulidi ya Mtume, Shaykh ´Abdul-Qaadir au mtu mwingine ni miongoni mwa Bid´ah za maovu.

Kumheshimu Mtume na kumpenda inakuwa kwa kumfuata yeye na Shari´ah yake Allaah (Ta´ala) amesema:

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

“Sema: “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni atakupendeni Allaah na atakusameheni dhambi zenu.” (03:31)

Kuwaheshimu watu wema na kuwapenda inakuwa kwa kuwafuata katika yale yenye kuafikiana na uongofu wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Sunnah zake.

Lililo la wajibu kwa waislamu ni wao washikamane na Sunnah za Mtume wao na Sunnah za makhaliyfah waongofu baada yao na mapokezi yao. Sambamba na hilo watahadhari na kuvuka mipaka kwa watu wema na kuwasifu kwa kupindukia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msinisifu kwa kupitiliza kama jinsi manaswara walivyofanya kwa mwana wa Maryam. Hakika mimi ni mja. Hivyo semeni “Mja wa Allaah na Mtume Wake”.”

Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake.

Amesema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Tahadharini na kuvuka mipaka katika dini. Hakika kilichowafanya kuangalia waliokuwa kabla yenu ilikuwa ni kuvuka mipaka.”

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/198-202)
  • Imechapishwa: 23/08/2020