Swali: Tumesoma kuwa watu wa Nuuh walitundika picha kwa ajili ya kumbukumbu. Leo baadhi ya chaneli zinatundika picha za wanachuoni na wanazikariri kwa njia ya picha kubwa iliyotundikwa kwenye kuta. Ni yapi maoni yako kuhusu hilo?

Jibu: Nyinyi mnajua kuwa TV nyingi leo zimewekwa kwa ajili ya kupotosha watu na kueneza shirki na njia zake, uchawi na njia zake na ukuhani. Msishangazwe kuona wanaeneza utundikaji wa picha za watu wenye kuadhimishwa ili waweze kuwafitinisha watu kwazo. Mjinga akiona hivo na yeye anakimbia kuitundika nyumbani kwake kama alivoona kwenye TV. Haya ndio makusudio: kuwalingania watu kwenye upotevu. Waislamu watahadhari na hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (20) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-2-15.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020