Nyimbo na muziki ni Qur-aan ya shaytwaan

Swali: Maneno Yake (Ta´ala):

وَأَنتُمْ سَامِدُونَ

“Na hali nyinyi ni wenye kupoteza muda kwa [mambo ya] ovyo.” (53:61)

Je, ni sahihi kuitumia kama dalili juu ya kuharamisha nyimbo na alama za michezo?

Jibu: Ndio. Wameitumia kama dalili juu ya kuharamisha nyimbo na kwamba wale wanaojishughulisha na nyimbo wamejitosheleza na Qur-aan. Nyimbo ni Qur-aan ya shaytwaan. Imaam Ibn-ul-Qayyim anasema katika “an-Nuuniyyah”:

Kwenye moyo wa mja hakukusanyiki

kupenda nyimbo na kupenda ala za nyimbo

Yule mwenye kupenda nyimbo hapendi Qur-aan. Na yule mwenye kupenda Qur-aan hapendi nyimbo. Haviwezi kukutana hivi viwili kwenye moyo wa muumini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (20) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-2-15.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020