Swali: Mimi natoka India na niko katika madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ninaposafiri katika nchi yangu sihudhurii swalah ya mkusanyiko msikitini kwa sababu imamu wa msikitini anaomba badala ya Allaah na anawaomba uokozi wafu. Badala yake ninaswali mkusanyiko na mke na watoto wangu nyumbani. Ninapata dhambi kwa kufanya hivo?

Jibu: Hili ndio la wajibu kwako ya kwamba usiswali nyuma ya mshirikina anayemuomba asiyekuwa Allaah. Kwa kuwa swalah yake ni batili. Ikiwa hukuweza kumbadilisha imamu huyu kwa kuweka imamu wa Tawhiyd, tokeni wewe na wenzako katika watu wa Tawhiyd na mjenge msikiti au mahala pa kuswalia [Muswallaa]. Ikiwa huna wenzako katika watu wa Tawhiyd katika majirani zako swali na mke wako na watoto zako mpaka pale Allaah (Jalla wa ´Alaa) ataposahilisha kuwepo kwa imamu katika watu wa Tawhiyd.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (20) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-2-15.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020