Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

07- Abu Ruqayyah Tamiym bin Aws ad-Daariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Dini ni nasaha.” Tukauliza: “Kwa nani?” Akasema kwa Allaah, Kitabu Chake, Mtume Wake, kwa wiongozi wa waislamu na watu wa kawaida.”

Miongoni mwa nasaha kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) ni kumpenda (Jalla wa ´Alaa), kufuata maamrisho Yake, kufuata Shari´ah Yake, kusadikisha khabari Zake na mtu awe ni mwenye kumkimbilia kwa moyo wake kwa kumtakasia Yeye Dini. Kumtakasia ´ibaadah, sawa kwa maneno na vitendo, ni haki ya Allaah (Jalla wa ´Alaa). Yule mwenye kuingiwa na kitu kwenye moyo wake ikawa kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, kama mfano wa kujionyesha au kutaka kusikika, hakutekeleza haki ya Allaah (Jalla wa ´Alaa).

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 160
  • Imechapishwa: 10/05/2020