Swali: Ni nini maana ya Hizbiyyah? Nini maana ya kwamba fulani ana Hizbiyyah? Ni kina nani Hizbiyyuun? Ni ipi Da´wah yao? Ni upi mfumo wao?

Jibu: Kila mwenye kwenda kinyume na mfumo wa Salaf ni katika mapote potevu. Hizbiyyah [sio katika] masharti yake ule mpangilio. Allaah (Jalla wa ´Alaa) ameziita nyumati zilizotangulia makundi أحزابا na amewaita Quraysh pindi walipokusanyika na waliokuwa pamoja nao ´makundi`. Hawakuwa na mpangilio wala hawakuwa na kitu. Sio katika masharti ya kipote kiwe kimepangiliwa. Endapo kitakuwa kina mpangilio basi ubaya wake utakuwa umezidi. Kuwa na ushabiki juu ya fikira maalum inayoenda kinyume na Qur-aa na Sunnah na kujenga mapenzi na chuki juu yake huku ni kujenga ukundi. Huku ni kujenga ukundi hata kama haukupangiliwa. Kuunda fikira iliyopinda na watu wakakusanyika juu yake hiki ni kipote sawa kiwe kimepangwa au hakikupangwa. Mambo ni hivyo midhali kinaenda kinyume na Qur-aan na Sunnah. Hiki ni kipote. Makafiri waliokuwa wakimpiga vita Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawakuwa na mpangilio huu uliyopo hii leo. Pamoja na hivyo Allaah aliwaita kuwa ni mapote. Kwa nini? Kwa kuwa walijifanya ukundi kwa batili wakiipiga vita haki:

كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَالْأَحْزَابُ مِن بَعْدِهِمْ ۖ وَهَمَّتْ كُلُّ أُمَّةٍ بِرَسُولِهِمْ لِيَأْخُذُوهُ ۖ وَجَادَلُوا بِالْبَاطِلِ لِيُدْحِضُوا بِهِ الْحَقَّ فَأَخَذْتُهُمْ ۖ فَكَيْفَ كَانَ عِقَابِ

“Walikadhibisha kabla yao watu wa Nuuh na makundi baada yao na kila ummah ulitilia hima kufanya njama juu ya Mitume wake ili wamkamate na wakabishana kwa ubatilifu ili waitengue haki [lakini hata hivyo] Nikawakamata. Basi ni vipi ilikuwa ikabu Yangu!” (40:05)

Allaah (Ta´ala) amewaita mapote pindi Quraysh, Ghatwafaan, Quraydhwah na makabila mengine walipokusanyika. Hawakupanga mpangilio huu. Walikusanyika na Allaah akawaita mapote na Suurah yenyewe ikaitwa Suurah “al-Ahzaab”. Sio katika masharti ya kipote kiwe kimepangiliwa. Wakiamini fikira ya batili, wakawa tayari kugombana kwa ajili yake, wakajadili kwa ajili yake na wakasimama upande wake hiki ni kipote. Wakizidisha juu ya hayo mpangilio, wanajeshi na mali inakuwa ni Hizbiyyah ya kihakika na wanakuwa ni katika mapote potevu.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf-us-Sitaar, uk. 18
  • Imechapishwa: 13/11/2016