Mwanamke Amemtukana Allaah Wakati Wa Ghadhabu Nyingi

Swali: Kuna mwanamke amemtukana Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) wakati alipokuwa katika hali ya ghadhabu. Mwanamke huyo ameolewa. Ni yapi ya wajibu kwake ili aweze kutubia?

Jibu: Ikiwa alishikwa na ghadhabu nyingi kiasi cha kwamba hajui kile anachokisema hakuna juu yake kitu kwa kuwa hakuwa ni mwenye kutambua hilo. Ama ikiwa alikuwa anatambua ni juu yake kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) na amuombe msamaha. Allaah anamsamehe yule mwenye kutubia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (04) http://alfawzan.af.org.sa/node/2047
  • Imechapishwa: 13/11/2016