Swali: Ni wepi mawalii wa Allaah?

Jibu: Ni waumini. Na nyinyi – Allaah akitaka – ni katika wao. Tunamuomba Allaah atujaalie sisi na nyinyi katika wao. Kila yule ambaye anamtii Allaah na Mtume Wake na akawa na msimamo juu ya haki ni walii wa Allaah. Tunamuomba Allaah atujaalie sisi na nyinyi katika wao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 40
  • Imechapishwa: 13/11/2016