Kwanini unamswalia Mtume na kizazi chake bila ya Maswahabah?

Swali: Mara nyingi tunamsikia Shaykh wakati anapomtaja Mtume basi husema:

صلى الله عليه وآله وسلم

“Swalah na salamu zimwendee yeye, kizazi chake… “

na wala hawataji Maswahabah zake. Je, ni katika matamshi yaliyopokelewa? Ni matamshi yepi ambayo ni bora na yaliyotangaa?

Jibu: Mimi sisemi:

صلى الله عليه وآله وسلم

“Swalah na salamu zimwendee yeye, kizazi chake… “

Bali nasema:

صلى الله عليه وعلى آله

“Swalah na salamu zimwendee yeye, juu ya kizazi chake… “  

Ni kitu gani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichowaambia Maswahabah zake wakati walipomwambia: “Tufunze ni vipi tukuswalie?” Aliwaambia waseme:

اللهم صل على محمد وعلى آل محمد

“Ee Allaah! Mswalie Muhammad, juu ya kizazi cha Muhammad… “

Wanachuoni wamesema kwamba kizazi cha Nabii ni wale wafuasi wake katika dini.

Muulizaji: Kadhalika katika Tashahhud?

Ibn ´Uthaymiyn: Kadhalika katika Tashahhud:

اللهم صل على محمد وعلى آل محمد

“Ee Allaah! Mswalie Muhammad, juu ya kizazi cha Muhammad… “

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (73) http://binothaimeen.net/content/1712
  • Imechapishwa: 20/04/2020