Kutofautiana kwa Salaf juu ya kwamba Allaah huiacha ´Arshi wakati wa kushuka

Allaah anapoteremka huiacha ´Arshi Yake au hapana? Hili ni suala ambal wale wenye kuthibitisha sifa wametofautiana kwalo. Wako waliosema kuwa haiachi ´Arshi Yake. Hayo yamenukuliwa kutoka kwa Imaam Ahmad bin Hanbal katika barua yake kwenda kwa Musaddad na kutoka kwa Ishaaq bin Raahuuyah, Hammaad bin Zayd, ´Uthmaan bin Sa´d ad-Daarimiy na wengineo.

Wapo wengine waliopinga hilo na wakasema kuwa barua kutoka kwa Ahmad bin Hanbal imepokelewa na mtu asiyejulikana.

Maoni ya kwanza ni yenye kutambulika kwa wanachuoni kama vile Hammaad bin Zayd, Ishaaq bin Raahuuyah na wengineo. al-Khallaal amepokea katika “as-Sunnah” kupitia kwa Sulaymaan bin Harb ambaye amesema:

“Bishr bin as-Sarriy alimuuliza Hammaad bin Zayd: “Ee Abu Ismaa´iyl! Hadiyth inayosema “Allaah hushuka katika mbingu ya dunia ya chini” – huhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine?” Hammaad bin Zayd akanyamaza. Kisha akasema: “Yuko mahala pake na anawakaribia viumbe Wake Atakavyo.”

Ibn Battwah amepokea kupitia kwa Ishaaq bin Raahuuyah ambaye amesema:

“Niliingia kwa ´Abdullaah bin Twaahir na kusema: “Ni Hadiyth aina gani mnazopokea?” Nikajibu: “Zipi, Allaah asahilishe jambo.” Akasema: “Mnapokea kwamba Allaah hushuka katika mbingi ya chini ya dunia.” Ndipo nikasema: “Ndio. Imepokelewa na waaminifu ambao wanapokea hukumu.” Akauliza: “Hushuka na akaiacha ´Arshi Yake?” Nikajibu: “Anaweza kuteremka pasi na kuiacha?” Akajibu: “Ndio.” Ndipo nikasmea: “Ni kwa nini basi unazungumza hili?”

Vilevile al-Lalakaa-iy ameyapokea haya kwa cheni ya wapokezi iliokatika na kwa tamko linaloenda kinyume na hili. Cheni ya wapokezi hii ni Swahiyh zaidi. Upokezi huu na ule ulio kabla yake ni zote mbili ni Swahiyh na zimepokelewa na maimamu waaminifu. Hammaad bin Zayd amesema kuwa yuko mahali pake na anawakaribia viumbe Wake atakavyo. Hapa amethibitisha kuwakaribia Kwake viumbe Wake pamoja na kwamba yuko juu ya ´Arshi Yake.

Kuhusiana na ´Abdullaah bin Twaahir, ambaye ni mbora katika watawala wa Khuraasaan, alikuwa akitambua kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi. Lakini hata hivyo akatatizwa na kwamba wakati huohuo anashuka, jambo ambalo kwa mtazamo wake linapelekea kuwa huiacha ´Arshi. Ndipo Imaam Ishaaq bin Raahuuyah akaafikiana naye kwamba yuko juu ya ´Arshi na akasema kumwambia:

“Anaweza kuteremka pasi na kuiacha?” Akajibu: “Ndio.” Ndipo nikasmea: “Ni kwa nini basi unazungumza hili?”

Hiyo ina maana kwamba ikiwa Yeye ni muweza wa kufanya hivo basi hialazimishi wakati anaposhuka kwamba huiacha ´Arshi. Hivyo haifai kupingana na ushukaji na kusema kwamba hiyo italazimisha kuwa huiacha ´Arshi. Upinganaji huu ni mwepesi kuliko upinganaji wa mwenye kusema kwamba juu ya ´Arshi hakuna kitu na matokeo yake akapinga mambo yote mawili.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Hadiyth-in-Nuzuul, uk. 40
  • Imechapishwa: 02/04/2019