Swali: Anayetia nia na akaazimia kula lakini akawa hakupata chakula. Je, anakuwa ni mwenye kufungua kwa kule kuazimia tu?

Jibu: Akikata nia katika swawm ya faradhi basi ameshafuturu. [Wanachuoni wa Fiqh wanasema]:

“Mwenye kunuia kula basi ameshafungua.”

Kwa kuwa amekata nia. Ama kuhusu swawm ya Sunnah hakuna neno, ikiwa hakula na kunywa, kule mtu kuwa na nia tu hakuiathiri swawm ya Sunnah. Kwa kuwa inasihi kwake kufunga kwa kutia nia kuanzia wakati wa mchana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (16) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-03-07.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014