06. Kosa la sita katika ´Aqiydah: Kusherehekea siku ya kuzaliwa

6- Kusherehekea siku ya kuzaliwa. Ni mamoja siku hiyo ni ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au ya mwenginewe. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakufanya hivo, makhaliyfah zake waongofu, Maswahabah wengine (Radhiya Allaahu ´anhum) wala wale waliowafuata kwa wema katika zile karne tatu bora. Ni jambo lililozuliwa katika karne ya nne na baada yake kwa sababu ya Faatwimiyyuun na wengineo katika Shiy´ah. Baadaye yakaja kufanywa na baadhi ya Ahl-us-Sunnah. Yote hayo ilikuwa ni ujinga juu ya hukumu za ki-Shari´ah na kuwafuata kichwa mchunga wale walioyafanya katika Ahl-ul-Bid´ah. Kwa hiyo ni lazima kujichunga kutokamana na hilo. Kwa sababu ni miongoni mwa Bid´ah zenye kukaripiwa zinazoingia ndani ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Tahadharini na mambo yaliyozuliwa. Hakika kila kilichozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”

Pia maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Yeyote mwenye kuzua katika dini yetu hii yale yasiyokuwemo atarudishiwa mwenyewe.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa).

Pia maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Yeyote mwenye kufanya kitendo kisichoafikiana na dini yetu  atarudishiwa mwenyewe.”

Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.

Pia maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Khutbah yake:

”Amma ba´d: Hakika mazungumzo bora ni Kitabu cha Allaah, uongofu bora ni wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), uovu wa mambo ni yale yaliyozuliwa na kila Bid´ah ni upotevu.”

Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake kupitia kwa Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Zipo Hadiyth nyingi kuhusiana na maudhui haya.

Jengine ni kwamba kusherehekea maulidi ni miongoni mwa njia zinazopelekea katika uchupaji mpaka na shirki. Hivyo ni lazima kutahadhari kutokamana na hilo na kuusiana kuyooka juu ya Sunnah na kuacha kwenda kinyume nazo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Akhtwaau fiyl-´Aqiydah, uk. 5
  • Imechapishwa: 02/08/2020