3172- ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza:

“Alikuwa akikwangura manii kutoka katika nguo yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na huku amesimama anaswali.”

Ameipokea Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyhah”: al-Hasan bin Muhammad ametuhadithia: Ishaaq ametuhadithia: Muhammad bin Qays ametuhadithia, kutoka kwa Muhaarib bin Dithaar, kutoka kwa ´Aaishah.

Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.

Hadiyth hii na mfano wake ni zenye kuafikiana juu ya kwamba manii ni kitu kisafi. Hadiyth hii iko wazi zaidi na ni dalili yenye nguvu. Isitoshe maoni yanayosema kuwa manii ni kitu kisafi ndio ya ash-Shaafi´iy, Ahmad na Ahl-ul-Hadiyht, tazama ”Fath-ul-Baariy”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (7/1/522)
  • Imechapishwa: 02/08/2020