Kuna muda kiasi gani kati ya daku na swalah ya Fajr?

Swali: Kulikuwa kuna muda kiasi gani kati ya daku na swalah ya Fajr?

Jibu: Wakati wa daku unaenda mpaka kuingia kwa alfajiri. Amesema (Ta´ala):

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ

“Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe wa alfajiri kutokana na uzi mweusi.” (02:187)

Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Bilaal anaadhini usiku. Hivyo kuleni na kunyweni mpaka aadhini Ibn Umm Maktuum.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Ibn Umm Maktuum alikuwa ni kipofu na haadhini mpaka aambiwe kumepambazuka. Imependekezwa kuchelewesha daku.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah al-Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

[1] Maalik (01/74), Muslim (02/768), at-Tirmidhiy (203) na wengineo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daa’imah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Ladjnah ad-Daa’imah (5611)
  • Imechapishwa: 26/04/2020