Kumpasua mwanamke ambaye kafariki na tumboni mwake kuna mtoto hai


Swali: Lau mwanamke anakufa na tumboni mwake ana kipomoko ambacho kiko hai. Je, inajuzu kwa daktari kupasua tumbo lake?

Jibu: Sioni kama kuna makatazo yoyote ya hili, hakuna ubaya – Allaah akitaka – kupasua tumbo lake na kumtoa mtoto nje.

Muulizaji: Baadhi yao [madaktari] wanawaua.

al-Waadi´iy: Kuwaua haijuzu. Haijuzu kumuua mtoto.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=381
  • Imechapishwa: 16/09/2020