Swali: Je, inafa kulipa Sunnah ya Rawaatib baada ya kupita wakati wake au inakuwa yenye kudondoka?

Jibu: Inakuwa yenye kudondoka ukipita wakati wake isipokuwa Sunnah ya Fajr. Hiyo inalipwa baada ya swalah au baada ya kuchomoza kwa jua. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake waliilipa pamoja na swalah ya Fajr wakati walipopitiwa na usingizi wakakosa Fajr katika baadhi ya safari zao. Isitoshe yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha ambaye atapitwa na Sunnah ya Fajr ailipe baada ya kuchomoza kwa jua. Isitoshe yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwona ambaye anailipa punde tu baada ya Fajr na hakumkemea kutokamana na hilo.

Vivyo hivyo Raatibah ya Dhuhr. Bora ikimpita mtu basi ailipe baada ya swalah ya Dhuhr pamoja na Raatibah ya baada yake. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliilipa baada ya swalah wakati ilipompita.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/384)
  • Imechapishwa: 10/11/2021