Hekima ya kubadilisha mahali pa Sunnah baada ya kuswali faradhi

Swali: Ni ipi hekima mswaliji anapomaliza kuswali na akataka kuswali Sunnah anabadilisha pahali pale na kwenda mahali pengine ambapo hakuswali faradhi?

Jibu: Haikuthibiti kuhusu kubadilisha mahali Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokana na ninavojua. Kumepokelewa juu ya hilo baadhi ya Hadiyth dhaifu.

Baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa hekima ya hilo – endapo tutasema kuwa ni jambo limewekwa katika Shari´ah – ni kutoa ushuhuda wa maeneo ambayo ameswalia. Allaah ndiye anajua zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/379)
  • Imechapishwa: 10/11/2021