Kuipa nyongo dunia kwa mujibu wa al-Baswriy

Aliulizwa al-Hasan [al-Baswriy]:

“Ni nani mwenye kuipa nyongo dunia?”

Akasema:

“Ni nani mwenye kuipa nyongo dunia ni yule ambaye akiwaona wengine anafikiria kuwa wao ni bora kuliko yeye.”

Hii ni maana kubwa aliyoichagua al-Hasan (Rahimahu Allaah). Mwenye kuipa nyongo dunia akimuona muislamu anafikiria kuwa ni bora kuliko yeye mbele ya Allaah (Jalla wa ´Alaa). Hili ni kwa sababu hakuufungamanisha moyo wake na dunia. Ameunyenyekeza moyo wake kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Sio mwenye kujinyanyua mbele ya watu.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 436
  • Imechapishwa: 13/05/2020