Watu wote wanampenda Allaah – vipi Yeye?

Waja wanaompenda Allaah (´Azza wa Jall) ni wengi. Bali kila mtu wa ´ibaadah, sawa ikiwa ni kwa batili au kwa haki, hakuwa ni mtu wa ´ibaadah isipokuwa ni kwa sababu anampenda Allaah (Jalla wa ´Alaa). Sio hili ndio linawapambanua watu. Kinachowapambanua watu mbele ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) ni: ni nani anayependwa na Allaah (Jalla wa ´Alaa). Baadhi ya maimamu wa Salaf wamesema:

“Kinachozingatiwa sio wewe kupenda. Kinachozingatiwa ni wewe kupendwa.”

Anachokusudia ni kwamba, mja kumpenda Mola Wake (Jalla wa ´Alaa) kunapatikana sawa kwa kuafikiana na yale Anayotaka Allaah au kinyume chake.

Manaswara wanampenda Allaah. Mayahudi wenye dini wanampenda Allaah. Watu wa dini mbali mbali wanampenda Allaah. Watu wa dini miongoni mwa waislamu ambao ni wajinga wanampenda Allaah. Lakini watu hawa sio wenye kupendwa kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Isipokuwa ikiwa kama watatekeleza yale anayoyapenda Allaah (Jalla wa ´Alaa) na kuyaridhia miongoni mwa maneno na matendo.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 430
  • Imechapishwa: 13/05/2020