Kufunua uso wa maiti wakati wa kumweka mwanandani

Swali: Je, inajuzu kumwondosha maiti kitambara cha usoni anapowekwa ndani ya kaburi lake ni mamoja maiti huyo ni wa kiume au wa kike?

Jibu: Hapana, hakuondoshwi kitu kutoka usoni mwa maiti, ni mamoja akiwa mwanamke au mwanamme. Anapowekwa mwanandani basi anaachwa kama alivyo na sanda yake. Hakuondoshwi kitu kutoka usoni mwake. Bali unafunikwa uso wake, ni mamoja akiwa maiti ni wa kike au wa kiume. Hakuna msingi wa kile kinachosemwa na baadhi ya wajinga kuhusu kufunua uso. Lakini kinachotakiwa kufanywa ni kufunguliwa mafundo na kuachwa mahali pake. Mafundo hayo yanatakiwa kufunguliwa na kuachwa mahali pake. Lakini usifunuliwe uso wake wala kiungo kingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4136/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%83%D8%B4%D9%81-%D9%88%D8%AC%D9%87-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%8A%D8%AA-%D8%B9%D9%86%D8%AF-%D9%88%D8%B6%D8%B9%D9%87-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%A8%D8%B1
  • Imechapishwa: 13/06/2020