Kutoka kiongozi wa vijana kwenda katika Khawaarij

Swali: Baadhi ya vijana huteua kiongozi katika mambo yanayokuwa kati yao. Wanapotaka kufanya jambo basi wanamuomba ruhusa yeye na wala hawawaombi ruhusa wazazi wao. Wanamfanya yeye ndio marejeo na wanaona kufanya hivo ni katika malezi. Ni ipi hukumu ya mtindo huu?

Jibu: Huu ni uzushi. Hiki ni kitu tunakijua tangu hapo kale. Wananikumbusha tukio lililotokea Makkah pindi kikosi cha wahudhuriaji waliokuwa pamoja nasi waliponiteua mimi kuwa kiongozi wao. Nikawaambia wamche Allaah. Nikawaambia kwamba hakuna kitu kinachoitwa uongozi katika hali ya mtu asipokuwa safarini. Kila ambapo mmoja wao anataka kufanya jambo basi wanamuomba idhini. Haya yalitokea miaka 25 huko nyuma. Baada ya hapo ikadhihiri kutoka kwa baadhi yao kwamba wana fikira za Khawaarij.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath-ur-Rahiym al-Waduud, uk. 260-261
  • Imechapishwa: 13/06/2020