Kufanyiana massage wanaume kwa wanaume na wanawake kwa wanawake

Swali: Unasemaje juu ya yale yanayofanywa na baadhi ya wasichana wao kwa wao au wavulana wao kwa wao wanafanyiana massage. Kwa mfano mtu anapanda juu ya tumbo lake na mwingine anamfanyia massage mgongoni mwake, ubavuni mwake, shingo yake, mabega yake, miundi yake na wakati mwingine mpaka mapaja yake. Mara hufanyika hayo nyuma ya nguo na mara hufanyika hayo moja kwa moja kwenye ngozi. Wakati mwingine huenda yule mwenye kukanda akatumia mafuta. Mambo kama haya yanafanyika kwa wingi khaswa katika vyuo vikuu kwa jinsia zote mbili.

Jibu: Hakuna neno ikiwa ni wanandoa ndio wenye kufanyiana hayo. Vovyote hali itakavyokuwa ni jambo linalofaa. Katika hali kama hii iwapo matamanio yake yatampanda ayakidhi. Kwa sababu yuko na mke wake.

Ama kufanya mambo haya kwa mtu mwingine ndani yake kuna fitina. Iwapo kijana atafanya hivo pamoja na kijana mwenzake, je, hakuna khatari matamanio yake yakampanda? Khatari ipo. Kadhalika iwapo mwanamke atafanya hivo kwa mwanamke mwenzake. Kwa sababu mwanamke hutamani kama  anavyotamani mwanaume. Sioni kuwa kitendo hichi kinafaa. Isipokuwa tu mume kwa mke wake.

Iwapo tutakadiria kuna mwanaume mzee mtumzima ambaye yuko na wasichana na akawaomba wamkande mgongo wake, haya hayana ubaya. Kwa sababu matamanio katika hali hii ni jambo liko mbali. Mwanaume mtumzima anahitajia kitu kama hichi. Kwa vile anahitajia na matamanio ni jambo liko mbali tunasema hakuna neno – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1492
  • Imechapishwa: 05/02/2020