Swali: Ni ipi hukumu ya kuwaiga wamagharibi katika mavazi na nguo zao kupitia magazeti ya mitindo?

Jibu: Haijuzu kwa waislamu wa kike na waislamu wa kiume kuwaiga wamagharibi na wamashariki katika mavazi yao maalum ambayo sio katika desturi za waislamu. Kwa sababu Allaah (Jalla wa ´Alaa) ametukataza kuigiliza tabia na kujifananisha na maadui zetu. Amesema (Ta´ala):

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ نَسُوا اللَّـهَ فَأَنسَاهُمْ أَنفُسَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ

“Na wala msiwe kama wale waliomsahau Allaah Naye akazisahaulisha nafsi zao – hao ndio mafasiki.”[1]

وَخُضْتُمْ كَالَّذِي خَاضُوا

”… na mkatumbukia katika upotofu na ukanushaji kama walivyotumbukia.”[2]

Wamesemwa vibaya na kutiwa kasoro kwa matendo yao kama walivosemwa vibaya maadui. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

“Punguzeni masharubu na zirefusheni ndefu – tofautianeni na washirikina.”

“Punguzeni masharubu na zirefusheni ndefu – tofautianeni na waabudia moto.”

Zipo Hadiyth zengine nyingi.

Kwa hiyo ni lazima kwa wanaume na wanawake wa Kiislamu kutojifananisha na maadui wa Allaah katika mavazi yao maalum na wajiepushe na hayo popote walipo kutokana na dalili zilizotangulia.

[1] 59:19

[2] 09:69

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/2966/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%AA%D9%82%D9%84%D9%8A%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D8%BA%D8%B1%D8%A8-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D8%B2%D9%8A%D8%A7%D9%89%D9%87%D9%85-%D9%88%D9%85%D9%84%D8%A7%D8%A8%D8%B3%D9%87%D9%85
  • Imechapishwa: 05/02/2020