Kufanya maulidi ni halali au haramu?

Swali: Je, kusoma mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni halali au haramu?

Jibu: Kufanya mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ya mwingine ni miongoni mwa Bid´ah zilizozushwa. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Mwenye kuzusha katika dini yetu hii yasiyokuwemo atarudishiwa mwenyewe.”

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (27/03)
  • Imechapishwa: 23/08/2020