Kuchelewesaha Twawaaf-ul-Ifaadhwah


Swali: Inafaa kuchelewesha Twawaaf-ul-Ifaadhwah na kuifanya siku ya tarehe kumi na tatu ambapo mtu akanuia pamoja nayo Twawaaf-ul-Wadaa´?

Jibu: Akichelewesha Twawaaf-ul-Ifaadhwah wakati wa safari ambapo akamaliza matendo ya hajj kama mfano wa kurusha vijiwe na unyoaji kisha Swafaa´ akatufu Twawaaf-ul-Ifaadhwah basi itamtosheleza kutokamana na Twawaaf-ul-Wadaa´.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 12/09/2020