Kubisha hodi kwa mtu zaidi ya mara tatu


Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuomba idhini inakuwa mara tatu.”

Je, naweza kubisha hodi zaidi ya mara tatu ikiwa ninamtaka rafiki yangu katika jambo ambalo ni muhimu na la kidharurah?

Jibu: Hapana. Udhahiri wa Hadiyth ni hapana. Unaweza kumrudilia kwa mara ya pili. Leo simu zimefanya kuweza kumpata mahala popote. Mtafute kwa njia ya simu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-11-02.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014