Swali: Je, inajuzu kuangalia chaneli ambazo kunarushwa ndani yake yale yanayofanywa na Raafidhwah siku ya ´Aashuuraa na kusikiliza Khutbah zao kwa ajili ya kushuhudia makosa na kutahadharisha nayo?

Jibu: Haijuzu kufanya hivo. Huenda ukasibiwa na kitu katika fitina au ukapata dhambi kwa wewe kuangalia maovu haya ilihali Allaah amekusalimisha nayo na amekuweka mbali nayo. Jitenge nayo mbali na usiyaangalie. Muombe Mola wako afya. Usijiaminishe nafsi yake na kusema mimi hakukhofiwi juu yangu khatari. Lau Mola wako angelitaka ungelikuwa kama wao. Moyo uko kati ya Vidole vya Mwingi wa rehema. Ni juu yako kumuomba Allaah afya na wala usiwaangalie. Usiangalie uzushi huu, maovu haya, shirki hii wanayomshirikisha nayo Allaah (´Azza wa Jall) na batili hii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2139
  • Imechapishwa: 12/07/2020