Msimamo kwa mzazi anayechelea kwa mvulana wake kwenda msikitini

Swali: Mtoto wangu wa kiume mwenye miaka 17 anapotoka kwenda kuswali mkusanyiko ninapokuwa sipo anarudi nyumbani amechelewa na ninakhofia juu yake na marafiki wabaya. Je, napata dhambi nikimzuia na swalah ya mkusanyiko?

Jibu: Huenda ni dhana na wasiwasi wako tu. Maadamu upo mchunge. Ikiwa haupo acha wasia kwa jirani yako au ndugu yako amchunge. Maadamu nia yako ni wewe kumchunga basi Allaah (´Azza wa Jall) atakusaidia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2139
  • Imechapishwa: 12/07/2020